TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE YA KRIKETI YAIBUKA BINGWA WA MASHINDANO YA NIDA TEXTILES CUP - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, November 6, 2025

TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE YA KRIKETI YAIBUKA BINGWA WA MASHINDANO YA NIDA TEXTILES CUP

Timu ya Taifa ya wanawake ya Kriketi ya Tanzania imeibuka bingwa wa mashindano ya NIDA Textiles Cup yaliyofanyika kwa siku mbili katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, dhidi ya timu ya Taifa ya Canada.

Mashindano hayo, yaliyolenga kuimarisha mahusiano ya michezo na kukuza mchezo wa Kriketi nchini, yalihusisha timu hizo mbili za kitaifa katika mfululizo wa michezo ya kirafiki yenye ushindani mkubwa.

Katika hafla ya kufunga mashindano hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bi. Neema Msitha, alikuwa mgeni Rasmi na alikabidhi tuzo kwa washiriki mbalimbali waliotoa mchango mkubwa kufanikisha mashindano hayo, wakiwemo wachezaji, viongozi, na wadau wa Kriketi nchini.

Aidha, Bi. Msitha alimpongeza mdhamini mkuu wa mashindano hayo, NIDA Textiles, kwa mchango wao mkubwa katika kuinua michezo nchini, hususan Kriketi, akisisitiza kuwa ushirikiano wa sekta binafsi ni chachu muhimu katika maendeleo ya michezo nchini.

“NIDA Textiles wameonyesha mfano wa kuigwa kwa kuwekeza katika michezo. Ushirikiano huu unapaswa kuendelezwa ili kuinua vipaji na kukuza michezo wa kriketi kimataifa nchini,” alisema Bi. Msitha.

Mashindano haya yamekuwa ishara ya maendeleo chanya ya mchezo wa Kriketi nchini Tanzania na uthibitisho wa juhudi za pamoja kati ya Serikali na wadau wa michezo, na sekta binafsi katika kukuza na kuendeleza michezo nchini.



No comments:

Post a Comment