Na Jeremia Mwakyoma
DODOMA - NOVEMBA
Jamii imeaswa kuwa na utaratibu wa kuchunguza Afya zao kubaini ugonjwa wa Kisukari na kuachana na tabia bwete katika maisha zinazochangia kusababisha Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo ugonjwa wa Kisukari.
Rai hiyo imetolewa na Dkt. Ahmad Mohamed Makuwani Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ugonjwa wa Kisukari Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.
"Tunaadhimisha Siku ya Kisukari Duniani nia kubwa ikiwa kupambana na ugonjwa huu unaoleta madhara makubwa kwa kuwahimiza Wananchi kuwa na utaratibu wa kuchunguza Afya ili kubaini kama mtu una ugonjwa wa Kisukari uweze kufuata masharti na maelekezo ya Wataalamu ili kudhibiti athari za ugonjwa huo" alisisitiza Dkt. Makuwani.
Aliongeza kuwa ili kujiepusha na ugonjwa huo ni vizuri watu wakabadili mfumo wa maisha kwa kuacha tabia bwete badala yake kuwa na desturi ya kuishughulisha miili, kufanya mazoezi kuachana na ulaji usio wa Afya kwa kula vyakula bora kama inavyoelekezwa na Wataalamu wa Afya na Lishe.
Dkt. Makuwani alibainisha kuwa kumekuwa na ongezeko la Wagonjwa wa kisukari kutoka 814,449 Julai 2023 na kufikia Wagonjwa 863,942 Juni, 2025 sawa na asilimia 0.1%, wakati idadi ya Wagonjwa wenye Vidonda vya Kisukari nayo ikiongezeka kutoka 75,678 mwaka 2020 kufikia 93,114 mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 23 huku Serikali kwa kushirikiana na Wadau na Chama cha Kisukari Tanzania wakifanikiwa kufungua kliniki 34 kwa ajili ya Wagonjwa wa Kisukari na Vidonda vya Kisukari.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa BMH Prof. Abel Makubi amebainisha kuwa BMH inatarajia kuanzisha huduma za matibabu ya vidonda vya Kisukari (Diabetic Foot) hivi karibuni na magonjwa mengine ya kisukari yanayohitaji upasuaji, na kwa sasa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wataalamu yanaendelea huku akibainisha kuwa kwa sasa huduma hiyo ya Matibabu ya vidonda vya Kisukari bado haipo Mkoani Dodoma.
Nae Mkuu wa Idara wa Magonjwa ya Kisukari na Homoni wa BMH Dkt. Glory Ngajilo amesema katika kuadhimisha Kisukari mwaka huu wametoa huduma za uchunguzi kwa Wananchi na kuwapa elimu huku akisisitiza kuwa kuchunguza ugonjwa wa kisukari mara kwa mara ni muhimu kwani mtu unaweza kuwa na kisukari bila kujijua kwani kisukari hakioneshi dalili katika hatua za awali badala yake mtu ukapata madhara kwa kuchelewa kuchukua hatua.

No comments:
Post a Comment