MACHUMU MKURUGENZI MPYA WA MAWASILIANO IKULU, NYALANDU AKITEULIWA KUWA BALOZI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, November 19, 2025

MACHUMU MKURUGENZI MPYA WA MAWASILIANO IKULU, NYALANDU AKITEULIWA KUWA BALOZI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumatano Novemba 19, 2025 amemteua Bakari Steven Machumu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, akichukua nafasi ya Bi. Sharifa Nyanga ambaye imeelezwa kuwa atapangiwa majukumu mengine.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka kwa Vyombo vya habari imeeleza pia kwamba Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mwanahabari Tido Mhando kuwa Mshauri wa Rais, habari na mawasiliano.


Katika hatua nyingine Bw. Lazaro Samuel Nyalandu ameteuliwa na Rais Samia kuwa Balozi.

No comments:

Post a Comment