Na Oscar Assenga, PANGANI.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Rajab Abdurhaman amekabidhi kiasi cha Milioni 13.4 kwa vijana wa Kikundi cha Bodaboda cha Hatupoi Group chenye maskani yao Kivukoni wilayani Pangani ikiwa ni hatua ya kuunga mkono hotuba ya Rais Dkt Samia Suluhu kwa vitendo kuwakwamua kiuchumi.
.jpg)
Akizungumza wakati akikabidhi hundi ya fedha hizo kwa Mwenyekiti wa Bodaboda wilaya ya Pangani alisema kwamba ameamua kuwaunga mkono kuwalipia deni la mkopo la Milioni 13.4 ambalo walipaswa kulilipa katika marejesho yao yaliyobakia baada ya kupata mkopo wa asilimia 10 kutoka Halmashauri.
Alisema kwamba wamekwenda kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu na kumshukuru kwa vitendo kwa hotuba yake aliyoitoa wakati anazindua Bunge la aliongeza mambo mengi kwa mustakabali wa mzima wa maendeleo ya Tanzania.
“Kwa niaba ya wana CCM na Wananchi mkoa wa Tanga nichukue nafasi hii kumpongeza Rais Samia kwa hotuba yake iliyosheheni mwelekezo mpya wa Taifa la wakati akizundua Bunge la 13 kama alivyosema hotuba hiyo ilishehena mambo mengi amezungumzia amani,umoja wa kitaifa wa nchi na maridhiano katika nchi yetu ili amani iendelee kuwepo ”Alisema
Rajabu ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga alisema kwamba kiongozi huyo mkuu wa nchi amezungumzia mambo mengi na kila mtanzania na mwana Tanga ameisikia na amefarijika na kufurahisha wa hotuba hiyo.
Aidha alisema kwamba wao watu wa Tanga wanampongeza na kumshuruku kama alivyosema kwenye hotuba kuna mambo mengi na moja wapo ambalo mkuu huyo wa nchi amezungumzia ni suala la kuwanyanyua kiuchumi vijana na wakina mama katika Taifa hili.
“Lakini akaenda mbali zaidi kusema ataunda wizara maalumu itakayohusiana na vijana na wanaposema vijana wapo vijana wa kiume na wakike tunampongeza kwa kiliona hilo tunaamini kupitia wizara hiyo atakayoiunda changamto za vijana zinazowakabili zitapatiwa majawabu kwa wakati”Alisema
.jpg)
Aliongeza kwamba wanamatumaini makubwa kwamba changamoto za vijana kwenye ajira serikalini na ajira za kujiajiri wenyewe na ajira za sekta binafasi zinakwenda kupatiwa majawapo kwa kwa muda mfupi.
.jpg)
Rajabu alisema kwamba ameamua kuwaunga mkono kama walivyosema walichukua mkopo halmashauri kwa mujibu wa mkataba miezi 16 mwaka mmoja na miezi minne na wanatakiwa kila tarahe 16 kila mwezi wawe wanarudisha kila walichoelekezwa na wameshalipa miezi 8 hivyo wamekwenda kuunga mkono hotuba ya rais kuhusu vijana na uchumi kwa vitendo
Akisoma Risala ya Kikundi cha Hatupoi Bodaboda Group alisema kwamba kilianzishwa mwaka 2020 wakiwa na wanachama na wanachama 10 na walipata cheti cha utambuzi kutoka wilaya ya Pangani .
Alisema baada ya kupata cheti hicho waliomba mkopo halmashauri kutoka fedha za asilimia 10 na hivyo kuweza kukopeshwa kiasi cha milioni 27,592,000 kwa ajili ya kununua pikipiki kwa ajili ya kuendesha mradi wa bodaboda.

Alieleza baada ya kupokea mkopo huo walikuwa wakirejesha kwa miezi 16 na ukomo wake ukiwa ni mwakani 2026 na kila mwezi rejesho ni 1,724,500 ambapo kupitia fedha hizo waliweza walinunua pikipiki 8 na mafuta ya kuanzia kazi na nauli za wajumbe kwenda kununua .
Hata hivyo alieleza baada ya kuanza kazi kwa muda wa miezi nane walifanikiwa kurejesha Milioni 14,152,000 na kubaki deni la Milioni 13,540,000 huku akieleza mafanikio mbalimbali walioyapata ikiwemo kutoa ajira za vijana 8,usimamizi wa fedha na kufanikiwa kurejesha fedha hizo .
“Tunamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu katika hotuba yake ya kulizundua Bunge baada ya kueleza kutakuwa na idara itakayosimamia vijana hivyo itawasaidia sana hivyo tunampongeza”Alisema
Kwa upande wake Mkuu wa dara ya Maendeleo ya Jamii Pangani Sekela Mwalukasa alisema kwamba wanajivunia uwepo wa kikundi hicho ambacho kimekuwa cha mfano huku akieleza Serikali ni sikivu imeweza kuja na mkakati wa kuwatoa vijana ili waweze kujikwamua kichumi kwa kutoa mikopo hiyo ya asilimia 10 ambayo haina riba inayotolewa kwa vijana na watu wenye ulemavu.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoa wa Tanga Mohamed Chande alimpongeza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Rajabu Abdurhamn kwa juhudi kubwa na Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu kwa kazi nzuri ya kutenga wizara ya vijana na fedha zinazotoka za mikopo sio za bure lazima zirejeshwe na vijana wapo tayari na kumpongeza mwenyekiti wa Bodaboda kwa kusimamia wilaya yake vizuri.
Mwisho.
.jpg)

.jpg)

No comments:
Post a Comment