MGODI WA BARRICK NORTH MARA WAZIDI KUPATA MAFANIKIO KATIKA UZALISHAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, November 12, 2025

MGODI WA BARRICK NORTH MARA WAZIDI KUPATA MAFANIKIO KATIKA UZALISHAJI

*Wavuka lengo la uzalishaji kwa asilimia 3% robo tatu ya mwaka

***

Mgodi wa Barrick North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara unaoendeshwa kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals Corporation, umezidi kupata mafanikio ya uzalishaji miongoni mwa migodi ya kampuni ya Barrick iliyopo barani Afrika kwa kuweza kuvuka lengo la matarajio yaliyowekwa kwa asilimia3% na kuchangia mafanikio ya ongezeko la uzalishaji katika kanda ya Afrika kwa ongezeko la asilimia 8% katika robo tatu ya mwaka.

Mafanikio haya yametokana na ufanisi katika uchimbaji kwenye mashimo yake ya wazi na chini ya ardhi ikiwemo mikakati ya kupunguza gharama za uchimbaji na uendeshaji wa mgodi kwa weredi mkubwa.

Haya yamebainishwa katika ripoti ya utendaji wa kampuni ya robo ya tatu ya mwaka 2025 iliyoishia Septemba 30 ya kampuni ya Barrick Gold Corporation iliyowasilishwa na Afisa Uendeshaji Mkuu na Rais na Afisa Mtendaji mkuu wa muda wa Barrick Mark Hill nchini Canada  ambayo imeeleza kwa kina hali ya utendaji katika katika kipindi hiki na uendeshaji wa migodi yake ulivyo katika nchi mbalimbali duniani.

Ripoti imebainisha vipimo vya kipekee vya utendakazi vinatoa picha ya kuvutia ya utendaji bora.Mapato kabla ya riba,kodi,upunguzaji thamani na matumizi ya mtaji (EBITDA) inayohusishwa barani Afrika iliongezeka kwa 65% robo hadi robo na gharama za uendeshaji zimepungua katika migodi hali ambayo imewezesha kupatikana kwa faida.

Mgodi mingine ya Barrick Mining Corporation ambayo imeweka rekodi nzuri ya utendaji barani Afrika ni Kibali uliopo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao umeongoza kwa kupata mafanikio ya ongezeko kubwa la 15% la uzalishaji katika robo ya tatu na kuwa mchangiaji mkuu zaidi katika ukuaji wa jumla wa eneo hili.

Kwa upande wa mgodi wa Lumwana uliopo nchini Zambia licha ya kusimamisha uzalishaji kwa ajili ya matengenezo katika robo ya tatu ambayo yalisababisha kushuka kwa uzalishaji kwa asilimia 7% bado uliendelea kuwa katika nafasi nzuri ya kukidhi mwongozo wa uzalishaji wa mwaka mzima.

Ripoti imebanisha zaidi kuwa operesheni za Barrick barani Afrika zimesalia katika nafasi nzuri ya kufikia mwongozo wa uzalishaji wa mwaka mzima licha ya changamoto za kikanda nchini Mali.

 Mchanganyiko wa utendakazi wa kipekee katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania umeweza kukabiliana kikamilifu na changamoto hizo kufanikisha malengo ya jumla ya uzalishaji wa kikanda na imani ya soko.

Katika  ripoti ya jumla ya kampuni imebainishwa kuwa Barrick Mining Corporation ilizalisha wakia 829,000 za dhahabu na tani 55,000 za shaba katika robo ya mwaka na ilizalisha mapato ya dola bilioni 4.1 pamoja na matumizi ya gharama za uendeshaji ya dola bilioni 2.4.  na dola bilioni $1.5 katika mzunguko.1 Mapato halisi kwa kila hisa ya $0.76 na mapato halisi yaliyorekebishwa kwa kila hisa1 ya $0.58 yaliongezeka kwa 62% na 23%, kutoka kipindi cha robo ya pili.

No comments:

Post a Comment