MTAA WA SEGU CHINI - NALA WAIOMBA DUWASA KUONGEZA MTANDAO WA MAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, November 27, 2025

MTAA WA SEGU CHINI - NALA WAIOMBA DUWASA KUONGEZA MTANDAO WA MAJI


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imeshiriki Kikao cha Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Segu Chini, Kata ya Nala Jijini Dodoma.

Katika kikao hicho, Viongozi wa Mtaa wameomba DUWASA iongeze Mtandao wa Maji katika Mtaa wao ili wananchi waweze kuunganishiwa maji majumbani mwao tofauti na sasa, ambapo huduma ya maji inapatikana katika vichoteo.

Viongozi hao wa Mtaa, pia wameitaka DUWASA kumalizia kazi ya kuviendeleza vichoteo vipya vilivyojengwa na Mkandarasi ili viweze kutumika na wananchi.

Akitolea ufafanuzi hoja za viongozi hao kwa niaba ya Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira wa DUWASA, Mhandisi Festo Mangimba amesema DUWASA bado inaendelea na utekelezaji wa Mradi na Mkandarasi atamalizia kazi iliyobaki.

Aidha, Mhandisi Mwangimba, amesema DUWASA inalaani vitendo vya uharibifu wa Miundombinu ya Maji katika Mtaa huo vinavyofanywa na wananchi wenye nia ovu ya kurudisha nyuma jitihada za serikali za kuwafikishia huduma ya maji wananchi wake, na kuwaomba Viongozi kushirikiana katika kulinda miundombinu ya maji ili isiharibiwe na ikibainika mwananchi amekamatwa kwa kosa la uhujumu miundombinu ya maji atashtakiwa kwa mujibu wa sheria.

No comments:

Post a Comment