SERIKALI KUIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, November 15, 2025

SERIKALI KUIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

Rais wa wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ili kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali za nchi pamoja na kupata huduma wanazostahili, wataelekeza jitihada kwenye mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi, ubadhirifu, uzembe, ukosefu wa nidhamu na ukosefu maadili. 


Dkt. Samia ameyabainisha hayo Jijini Dodoma wakati akilihutubia Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuongeza kuwa msingi wa mafanikio hayo ni utawala wa sheria, uadilifu na uwajibikaji katika kila ngazi, kuanzia juu mpaka chini.


"Ni lazima tudhibiti wachache wanaotaka kuturudisha nyuma kwa kuendekeza maslahi binafsi,"amesema. 


Ameongeza kuwa ili kuimarisha uwajibikaji Serikalini, wataendelea kutekeleza programu za maboresho ya utumishi wa umma, ikiwemo matumizi ya mifumo ya upimaji wa utendaji kazi. 


"Wajibu huenda na haki, au haki huambatana na wajibu, hivyo basi, pamoja na kuwataka watumishi wa umma kuwajibika ipasavyo, tutaendelea kuboresha maslahi yao kadri uchumi utakavyoruhusu,"ameongeza. 

No comments:

Post a Comment