SERIKALI YAELEKEZA KUFUNGULIWA KWA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, November 24, 2025

SERIKALI YAELEKEZA KUFUNGULIWA KWA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameagiza kufunguliwa kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima huku akielekeza lipewe miezi sita ya uangalizi katika kuzingatia miiko, masharti na sheria za uendeshwaji wake.

Sambamba na hilo, ameelekeza kurekebishwa kwa sharti linalotaka kufungiwa kwa nyumba ya ibada iwapo atakosea kiongozi, akisisitiza kuwa anayekosea ndiye aadhibiwe bila kuathiri waumini kufanya ibada.

“Natambua ilikuwepo hii moja ya Ufufuo na Uzima kaifungulie, ifungulie wape masharti ya uangalizi ndani ya miezi sita. Ziandikie taasisi zote za kidini kuzikumbusha miiko na mipaka ya ufanyaji kazi, sawa sawa na sheria na Katiba ya nchi yetu,” amesema.

Kanisa hilo lilifutwa usajili Juni 2 mwaka huu kutokana na kukiuka masharti ya uendeshaji wake kwa kuhusisha siasa ndani yake.

Dkt. Mwigulu ametoa kauli hiyo Jumatatu, Novemba 24, 2025, alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara baada ya ziara ya kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na vurugu za Oktoba 29, 2025.

No comments:

Post a Comment