TANROADS NJOMBE YAENDELEA KUHAKIKISHA BARABARA ZINAPITIKA KIPINDI CHOTE CHA MVUA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, November 23, 2025

TANROADS NJOMBE YAENDELEA KUHAKIKISHA BARABARA ZINAPITIKA KIPINDI CHOTE CHA MVUA



Kwa mujibu wa maelekezo ya Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta, kwa Mameneja wa Mikoa yote kuhakikisha barabara zinabaki salama na kupitika kipindi hiki cha mvua, TANROADS Mkoa wa Njombe imeongeza kasi ya usimamizi na matengenezo katika maeneo yaliyoathiriwa na mvua.

Barabara ya Itoni–Ludewa–Manda (km 211.4), hususan Sehemu ya Pili ya Itoni–Lusitu (km 50) inayojengwa kwa kiwango cha zege, imefanyiwa matengenezo ya haraka baada ya changamoto za mvua ili kuhakikisha watumiaji wanaendelea kusafiri kwa usalama na uhakika.

Kazi zinaendelea mchana na usiku, kuhakikisha magari yanapita bila kukwama na shughuli za kiuchumi zinaendelea vyema katika mkoa wa Njombe.

Kwa kushirikiana, TANROADS Makao Makuu, ofisi ya TANROADS Mkoa wa Njombe, pamoja na mkandarasi, wamehamia barabarani kuhakikisha kila eneo linalohitaji uingiliaji linafanyiwa kazi mara moja.

Ujumbe kwa wananchi:
Serikali kupitia TANROADS inaendelea kuhakikisha barabara zote zinapitika msimu mzima wa mvua ili kuimarisha usafiri, usafirishaji na uchumi wa wananchi.







No comments:

Post a Comment