
Mashirika makubwa na maarufu ya ndege duniani kama Qatar na KLM yameendelea kupata abiria wengi wanaofanya safari zao kuja Tanzania kwa lengo kubwa moja tu la kutimiza ndoto za maisha yao kufika na kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini.
Haya yanaendelea kudhihirika kwa wingi wa wageni wanaoendelea kuingia nchini, mathalani, mnamo tarehe 20 na 21 Novemba 2025, Mamia ya watalii waliwasili nchini wakitokea nchi mbalimbali duniani kupitia ndege za mashirika ya Qatar na KLM.
Wengi wao wakieleza shauku zao za kupanda Mlima Kilimanjaro ambao wamekuwa wakisikia sifa zake kwa miaka mingi maishani mwao.
Wengi wanapofika nchini huvutiwa zaidi na hali ya amani na utulivu pamoja na watu waliojaa utu na ukarimu wa hali ya juu.







No comments:
Post a Comment