TFRA kuimarisha afya za wafanyakazi kupitia SHIMMUTA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, November 28, 2025

TFRA kuimarisha afya za wafanyakazi kupitia SHIMMUTA



Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imeendelea kuonesha ushiriki na utayari mkubwa katika Michezo ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) ya mwaka 2025, inayofanyika mkoani Morogoro.

Akizungumza leo tarehe 26 Novemba 2025, Mwenyekiti wa Michezo wa TFRA, Frank Kapama, amesema ushiriki wa Mamlaka katika mashindano hayo ni sehemu muhimu ya kujenga afya, kuimarisha umoja, kuongeza morali ya watumishi pamoja na kuhimarisha mazingira ya kufanya kazi kwa ushirikiano.

Aidha ,Kapama amebainisha kuwa michezo hiyo ni fursa ya kuimarisha mahusiano na taasisi nyingine za serikali na kuongeza ari ya utendaji katika maeneo ya kazi.

TFRA itashiriki michezo ya ndani na nje ikiwemo mpira wa kikapu kwa wanaume na wanawake,riadha,mpira wa wavu,pool table ,drafti, bao na darti

TFRA imewataka watumishi wake kuendelea kuonesha nidhamu, juhudi na ushindani chanya katika michezo yote, ili kuhakikisha wanapata mafanikio makubwa na kuibuka na ushindi katika mashindano ya SHIMMUTA 2025.


No comments:

Post a Comment