TIMU YA VOLLEYBALL YA WANAUME REA YAANZA KUGAWA KIPIGO SHIMMUTA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, November 27, 2025

TIMU YA VOLLEYBALL YA WANAUME REA YAANZA KUGAWA KIPIGO SHIMMUTA



Timu ya mpira wa wavu ya wanaume ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) kwa kishindo baada ya kuibuka na ushindi mkubwa dhidi ya timu ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA).

Katika mchezo uliochezwa leo Novemba 27, 2025 katika viwanja vya Bwalo Mkoani Morogoro, wachezaji wa timu ya REA walionyesha kiwango cha juu cha mchezo na kasi iliyowaduwaza wapinzani wao, na hivyo kuweza kuwagaragaza TFRA kwa ushindi wa seti 2 kwa 1.

Ushindi huu wa mwanzo unatoa motisha kubwa kwa timu ya REA kuelekea michezo mingine, huku wakiwa na matumaini ya kutwaa ubingwa katika mashindano hayo yanayoendelea mkoani Morogoro.

Kocha wa timu hiyo alieleza kuridhishwa na juhudi za wachezaji wake na kuahidi kuendelea kuweka mikakati imara ili kuhakikisha REA inasalia kileleni mwa kundi hilo gumu.

Timu hiyo ambayo imeshiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza imeonekana kuwavutia mashabiki wengi waliokuwa katika viwanja hivyo.

No comments:

Post a Comment