WAZIRI MCHENGERWA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAWEKEZAJI WAKUBWA WA DAWA DUNIANI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, November 28, 2025

WAZIRI MCHENGERWA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAWEKEZAJI WAKUBWA WA DAWA DUNIANI.


Na Mwandishi Wetu- Algeria

Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa amekutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali wa uzalishaji wa dawa na teknoloajia mbalimbali za afya ambapo wengi wao wameonesha shauku kubwa la kuwekeza nchini.

Amekutana na wadau hao katika maonesho makubwa barani Afrika yanayofanyika Algiers Algeria baada ya kuhudhuria Mkutano wa Mawaziri kuhusu Uzalishaji wa Ndani wa Dawa na Teknolojia barani Afrika unaoendelea nchini Algeria.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine unalenga kuimarisha sekta ya dawa na teknolojia ya afya barani Afrika kama ilivyoazimiwa wakati wa kikao cha 74 cha Shirika la Afya Duniani (WHO)- Kanda ya Afrika kilichofanyika Agosti 2024.

Akiwa anaongoza ujumbe wa tanzania, Mhe. Mchengerwa amefanya mazungumzo na wadau kadhaa ambao wengi wao wamevutiwa na kuwekeza katika maeneo mbalimbali ili kutoa huduma kwa gharama nafuu.

Aidha, wameonyesha kuridhishwa sera na mazingira mazuri ambayo Serikali imeyaweka.

Mhe. Mchengerwa amewahakikishia wawekezaji wote wenye dhamira ya kweli ya kushirikiana na Serikali katika uzalishaji wa dawa na teknolojia ya afya kwa masilahi mapana ya pande zote mbili wanakaribishwa.


"Sisi kama nchi tupo tayari kuwakaribisha wawekezaji makini ambao wapo tayari kuwekeza nchini". Amefafanua Mhe. Mchengerwa

Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zilizopewa kipaumbele katika mkutano huo kutokana na kuthamini uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu na kihistoria wa nchi hizo mbili.

Ikiwa ni takribani wiki tatu tangu ateuliwe na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Mhe Mchengerwa akiwa nchini Algeria anatarajia kutembelea maeneo mbalimbali ya mnyororo wa thamani ya sekta ya hiyo na kufanya mazungumzo.

No comments:

Post a Comment