
Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa, Abdallah Ulega na Naibu wake Mheshimiwa, Eng. Godfrey Kasekenya wamewasili katika ofisi za Wizara ya Ujenzi muda mfupi mara baada ya kuapishwa Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo tarehe 18 Novemba, 2025.
Katika hafla hiyo ya mapokezi, Waziri Ulega amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjalia uhai na afya njema, amemshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua tena kuiongoza Wizara ya Ujenzi na amewashukuru watumishi wote wa Wizara ya Ujenzi kwa ushirikiano waliowapa katika kipindi kilichopita.
“Katika kipindi hiki, Mheshimiwa Rais ametuelekeza tufanye kazi kwani anataka matokeo, hivyo tusimuangushe, tufanye kazi kwa bidii wakati wote zitakazoleta tabasamu kwa wananchi”, amesisitiza Waziri Ulega.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Kasekenya amewashukuru watumishi na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana ili waweze kuleta matokeo chanya kwa wakati na kufikia malengo kwa manufaa ya wananchi wote.










No comments:
Post a Comment