WAZIRI MKENDA NA NAIBU WAZIRI MHE. WANU KUENDELEZA MAGEUZI YA ELIMU NCHINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, November 18, 2025

WAZIRI MKENDA NA NAIBU WAZIRI MHE. WANU KUENDELEZA MAGEUZI YA ELIMU NCHINI


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda na Naibu Waziri Mhe. Wanu Hafidh Ameir wamesisitiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya elimu nchini.

Akizungumza baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara tarehe 18 Novemba 2025 jijini Dodoma, Prof. Mkenda ameeleza kuwa Wizara imejipanga kuhakikisha elimu inayotolewa inawawezesha vijana kupata maarifa, stadi stahiki na ujuzi ili waweze kujiajiri na kushindana katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi.

Waziri Mkenda ameongeza kuwa Wizara itasimamia kikamilifu elimu katika ngazi mbalimbali na kuweka mkazo katika mafunzo ya amali.


Kwa upande wake, Naibu Waziri Mhe. Wanu Hafidh Ameir ameahidi ushirikiano katika kufanikisha mageuzi hayo na amehimiza kuendeleza utamaduni wa ushirikiano na weledi katika kazi ili kuhakikisha malengo ya Serikali ya kutoa elimu bora kwa wote yanafanikiwa.


Mhe. Wanu na Prof. Mkenda walipokelewa rasmi katika ofisi za Wizara, ambapo watumishi walionesha mapokezi mazuri na ari ya kushirikiana katika safari ya mageuzi ya elimu.




Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amesema viongozi bora ni chachu ya utekelezaji wa mageuzi ya elimu nchini ambayo yatasaidia kupata wahitimu mahiri wenye uwezo wa kushiriki katika maendeleo ya taifa.


Prof. Nombo amewapongeza viongozi wapya Mhe. Mkenda na Mhe. Wanu, ambapo amesema kuwa uteuzi wao na kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni ishara ya kuaminiwa kwa uongozi wao mahiri.


Amesisitiza kuwa Wizara inajivunia viongozi hao na ipo tayari kushirikiana kikamilifu katika utekelezaji wa mageuzi ya elimu nchini.






No comments:

Post a Comment