Wizara ya Maji inawashirikisha wadau kuhusu kazi na matumizi ya mabwawa - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, November 21, 2025

Wizara ya Maji inawashirikisha wadau kuhusu kazi na matumizi ya mabwawa


Wizara ya Maji inawashirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali katika kuhakikisha usimamizi salama wa mabwawa na rasilimali za maji unafanyika kwa kiwango stahiki nchini.

Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali za maji Bw. Robert Sunday amesema hayo wakati akihitimisha mkutano wa mwaka wa usalama wa mabwawa uliofanyika jijini Mwanza.

Mkutano huo wa siku tatu umewahusisha wadau kutoka sekta ya umma na sekta binafsi kwa lengo la kujikumbusha na kuwa na uelewa wa tahadhari za mapema kuhusu mabwawa.

Amesema mabwawa ya maji na mabwawa ya tope sumu yanatakiwa kuhifadhiwa vizuri ili kuepuka majanga kwa maisha ya binadamu na mazingira kwa ujumla .

“Mkutano huu umekusanya wataalam na watunga sera kujadili changamoto zinazojitokeza, kubadilishana uzoefu, na kukuza utamaduni wa usalama na uwajibikaji” Bw. Sunday amesema.

Ameongeza mmiliki wa bwawa anapaswa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu kuanzia kazi ya usanifu, kujenga na kuendesha ili kuhakikisha bwawa linakuwa salama

Mchakato huo unahusisha wataalam walio sajiliwa na wenye uwezo wa usanifu na kutoa vibali vya ujenzi wa mabwawa ili kuepukana na athari na majanga yanayoweza kutokea kutokana na mabwawa hayo.





No comments:

Post a Comment