
Aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge lililopita na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan Zungu, amechaguliwa kwa kishindo kugombea nafasi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Novemba 9, 2025 jijini Dodoma, Zungu amepata kura 348 akimshinda mpinzani wake Stephen Masele aliyepata kura 16.
Kwa upande wa nafasi ya Naibu Spika, Mbunge Daniel Silo ameibuka kidedea baada ya kupata kura 362, huku wagombea wengine waliokuwa wamejitokeza awali wakijitoa kabla ya upigaji kura kuanza.
Kwa sasa, Zungu anasubiri wagombea wengine nje ya CCM kama watajitokeza kwa ajili ya kushindaniwa kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Jumanne, Novemba 11, 2025, ndani ya Ukumbi wa Bunge.

No comments:
Post a Comment