Akizungumza na waandishi wa habari leo Disemba 02, 2025 Mtendaji Mkuu wa ADEM Dkt. Maulid J. Maulid amewakaribisha wadau wote wanaojihusisha na masuala ya elimu nchini katika Mkoa wa Pwani na kwingineko nchini kuja kushiriki katika mbio hizo zitakazofanyika siku ya Jumamosi tarehe 06 Disemba, 2025 kuanzia saa 12 kamili Asubuhi ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Aboubakar Kunenge.
Pia kuhusu utaratibu wa namna ya kushiriki Dkt. Maulid amesema washiriki watachangia gharama kidogo ili kufanikisha lengo la Wakala la kukusanya fedha kwa ajilo ya kuboresha miundombinu yake na watapatiwa vifaa kwa ajili ya kushiriki mbio hizo ikiwemo jezi, kofia n.k huku washindi katika mbio hizo wakipatiwa zawadi mbalimbali za fedha taslimu.
Aidha, Dkt. Maulid amesema mbio hizo zitafanyika katika umbali wa Kilomita 10 na Kilomita 5 kuanzia ADEM Bagamoyo na kisha kuelekea katika viunga vya Mji huo mpya wa Bagamoyo kwa umbali uliotajwa. Aidha, amesisitiza wanaotaka kushiriki mbio hizo kuwasiliana na Wakala kwa Simu Namba: 0752 160555/0742 777222
Kauli mbiu ya mbio hizo inasema “Miundombinu Bora kwa Uongozi Thabiti wa Elimu” ikichagiza kuchangia uboreshaji wa miundombinu ya Elimu ili kuimarisha utoaji wa Elimu Bora.
















No comments:
Post a Comment