
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho,(Mb) tarehe 8 Desemba 2025, amefanya ziara ya Kikazi kwa kutembelea Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa, Chamwino mkoani Dodoma.
Ziara hiyo wa Waziri wa Ulinzi na JKT ni muendelezo wa ziara zake za kikazi alizozianza kwa ajili ya kujitambulisha na kuzungumza na Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma wa Wizara ya Ulinzi.
Mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya JKT, Dkt Rhimo Nyansaho alipokelewa na mwenyeji wake, Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele na uongozi mzima wa Jeshi la Kujenga Taifa.
Pamoja na mambo mengine katika ziara hiyo,Waziri wa Ulinzi na JKT alipata wasaa wa kupanda mti wa kumbukumbu na baadaye kuzungumza na Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma.
Katika hotuba yake, Dkt Rhimo Nyansaho amempongeza Mkuu wa JKT kwa mapokezi mazuri na kusema kuwa Serikali kupitia Wizara anayoiongoza itaendelea kuiwezesha JKT ili itekeleze ipasavyo majukumu yake ya Msingi ambayo ni Malezi ya Vijana, Uzalishaji Mali na Ulinzi wa Taifa kwa ujumla.




No comments:
Post a Comment