Dodoma
TANROADS Mkoa wa Dodoma inapenda kuujulisha umma kuwa kazi za marekebisho ya kipande cha majaribio cha barabara katika eneo la Makalavati, Wilaya ya Kongwa (barabara kuu ya Dodoma–Gairo) zimeanza rasmi kufuatia maelekezo yaliyotolewa.
Hatua hii ni sehemu ya taratibu za kitaalamu za kuhakikisha ujenzi wa barabara unazingatia viwango vilivyokubaliwa, ubora unaotakiwa na thamani ya fedha za umma. Mkandarasi anaendelea kutekeleza marekebisho hayo kwa karibu chini ya usimamizi wa TANROADS.
TANROADS itaendelea kutoa taarifa kwa umma kadri kazi zinavyoendelea.
Tuendelee kushirikiana kwa maendeleo ya miundombinu bora 🇹🇿🛣️





No comments:
Post a Comment