MBUNGE MAVUNDE AITAKA JAMII KUWAKUMBUKA NA KUWAJALI WAJANE NA YATIMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, December 20, 2025

MBUNGE MAVUNDE AITAKA JAMII KUWAKUMBUKA NA KUWAJALI WAJANE NA YATIMA



Na Mwandishi Wetu, 𝘿𝙤𝙙𝙤𝙢𝙖


Mbunge wa Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde ametoa rai kwa jamii kuwajali na kuwakumbuka yatima na wajane katika utatuzi wa changamoto zao mbalimbali na kuwapa faraja.

Mh. Mavunde ameyasema hayo leo wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Taasisi ya Joy of Giving ya kugawa mahitaji kwa wajane na yatima ikiwemo vyakula na mahitaji ya shule kwa watoto.

“Nawapongeza Joy of Giving Foundation kwa kuwajali na kuwakimbilia wahitaji mara zote.

Mmekuwa mfano mzuri kwenye jamii na hivyo mnatuma ujumbe kwa Jamii nzima juu ya kuwajali na kuwakumbuka wajane na yatima huku tukijua kwamba hii ni ibada kubwa.

Nitaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuwahudumia wajane na yatima na kwasasa tunatarajia kuwa na Tamasha kubwa la wahitaji la kila mwaka ili kutengeneza msingi wa utatuzi wa changamoto zao”Alisema Mavunde

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Joy of Giving Bi. Jackline Nitwa Machoke amesema Taasisi yake imejipanga kufanya tukio la mara moja kila mwaka la kuwahusu wajane na yatima na kutoa rai kwa wadau kuiwezesha Taasisi hiyo ili kuweza kutimiza malengo yake hasa katika huduma za kila siku za kuwahudumia watu wenye ugonjwa mbalimbali na upatikanaji wa bima ya Afya kwa wananchi wanaoishi katika mazingira magumu.

Hafla hiyo imehusisha watoto yatima na wajane takribani 200 ambao wote wamepatiwa mahitaji mbalimbali kutoka kwa Mbunge Mavunde na Taasisi ya Joy of Giving.







No comments:

Post a Comment