SHEMDOE AWATAKA WALIOKWENDA KUSHEHEREKEA KRISMASI VIJIJINI KUNUNUA BIDHAA ZA WENYEJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, December 25, 2025

SHEMDOE AWATAKA WALIOKWENDA KUSHEHEREKEA KRISMASI VIJIJINI KUNUNUA BIDHAA ZA WENYEJI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akitoa salamu za Krismass kwa watanzania, mara baada ya ziara yake ya kikazi aliyoifanya kwenye Soko la Kariakoo jijini Dar. Es Salaam.

Na James Mwanamyoto - Dar es Salaam


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewahimiza wananchi waliosafiri kutoka mijini kwenda vijijini, kuhakikisha wananunua bidhaa huko huko vijijini ili kuleta tabasamu na kuongeza mzunguko wa fedha vijijini.

Prof. Shemdoe ametoa wito huo katika salaam zake za Krismasi alizotoa Disemba 24, 2025, mara baada ya ziara yake ya kikazi aliyoifanya kwenye Soko la Kariakoo jijini Dar. es Salaam.

"Ndugu Watanzania wenzangu ambao tumefanikiwa kwenda kusherehekea Sikukuu ya Noel vijijini kwetu, tuhakikishe tunanunua bidhaa zinazopatikana vijijini huko huko kwa wenyeji wetu, ili tuwaachie tabasamu na kuunga mkono azma ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuinua kipato cha Watanzania,” amesisitiza Prof. Shemdoe.

No comments:

Post a Comment