
Mbunge wa Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde leo amekabidhi awamu ya kwanza ya madawati 2700 kwa ajili ya Shule za Sekondari za Jiji la Dodoma kufuatia maelekezo ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kutaka kukamilika kwa miundombinu ya madarasa na upatikanaji wa madawati ya kuwapokea wanafunzi wapya wa kidato cha Kwanza Januari 2026.
Mbunge Mavunde amelipongeza Jiji la Dodoma kwa hatua za makusudi za kuhakikisha upatikanaji wa madawati ya kutosha zaidi ya 2713 ili wanafunzi wasome katika mazingira bora.
“Hii ni hatua kubwa katika kuboresha sekta ya Elimu ndani ya Jiji la Dodoma kwa kuweka mazingira bora ya kusomea ya wanafunzi wetu”Alisema Mavunde
Akizungumza katika hafla hiyo fupi,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh. Jabir Shekimweri amesema ni wajibu wa watu wote kuyatunza madawati hayo ili yawafae wanafunzi wengi kwa siku zijazo.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Dkt. Fredrick Sagamiko amesema Jiji la Dodoma limejipanga kuhakikisha wanafunzi wote wanasoma katika mazingira rafiki na kwamba hatua ya utoaji wa madawati 800 leo ni hatua ya kwanza ya kukamilisha madawati 2713 ili kuwafikia kundi kubwa la wanafunzi wa Jiji la Dodoma.





No comments:
Post a Comment