
Na Hadija Omary Mazezele
Kesho Tarehe 17 Diemba 2025 Tanzania itashiriki mkutano maalumu kujadili muelekeo wa nchi katika utekelezaji wa maamuzi baada ya COP30.
Mshauri wa Rais kuhusu Masuala ya Mazingira na Mwenyekiti wa Kundi la Majadiliano la Afrika (AGN), Dkt. Richard Muyungi, amesema kikao hicho ni fursa ya kutafsiri maamuzi ya COP30 kuwa hatua za utekelezaji zinazoonekana kwa wananchi.
Dkt Mayungi amesema kuwa nchi inahitaji kuwa na mifumo bora ya utekelezaji kuliko ahadi ili kisaidia nchi masikini hasa zinazoendelea kupambana na athali za mabadiliko ya tabia nchi.
"Hatuhitaji tena kubaki kwenye ngazi ya ahadi pekee, bali tunahitaji mifumo madhubuti ya utekelezaji na uwajibikaji itakayohakikisha fedha za tabianchi zinafika kwa haraka na kwa uwazi kwenye jamii zinazobeba mzigo mkubwa wa athari za mabadiliko ya tabianchi, hususan nchi zinazoendelea.Amesema Mayungi.
Amesema Makubaliano yaliyofanya kwenye mkutano wa COP30 yanatoa fursa kwa nchi kupata kati ya dola milioni Tano hadi dola milioni 20 kwa kila mradi hivyo inapaswa kuimarisha mifumo ya uwajibikaji ili kuharakisha mifumo ya uwajibikaji na kuhakikisha fedha za tabia nchi zinafika kwenye jamii zaidi.

Baadhi ya wakulima na mkoani Tabora ambao baadhi yao walikiwa wakifuatilia mkutano wa COP30 wamesema maamuzi ya COP30 yazingatie hadi ngazi za chini kwani wamekuwa wakipata changamoto za tabia nchi serikali iwaangalie kwa jicho la tatu.
Kwa upande wake Yombo Mlokozi ambaye ni mkulima wa mazao ya chakula na biashara kwa mika 20 sasa kata ya Tuli manispaa ya Tabora ameeleza kufurahishwa na kikao kitakachokwenda kufanyika siku ya kesho huku matarajio yake ni kuona serikali namna gani inawawezesha wakulima wadogo teknolojia bora za kilimo zitakazowasaidia masika na kiangazi kukabiliana na tabia nchi.
"Tunafurahia kuona serikali ikikaa kujadili maamuzi ya COP30, lakini matarajio yetu kama wakulima wadogo ni kuona matokeo yake yakitafsiriwa kuwa teknolojia za kisasa kukabiliana moja kwa moja na mabadiliko ya tabianchi.” Amesema Yombo
Kwa ujumla, kikao cha kesho kinatajwa kuwa hatua muhimu ya Tanzania kuhamisha mjadala wa kimataifa wa tabianchi kutoka kwenye makubaliano ya maandishi kwenda kwenye utekelezaji unaogusa maisha ya wananchi. Wadau wakiwemo wakulima wadogo wanatazamia kuona maamuzi ya COP30 yakishuka hadi ngazi za chini, yakiboresha uzalishaji wa chakula, ustahimilivu wa jamii na kuchochea maendeleo jumuishi yanayozingatia haki ya tabianchi kwa wote.

No comments:
Post a Comment