DKT. MUYUNGI ATETA NA WATENDAJI WAANDAMIZI COSTECH - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, January 29, 2026

DKT. MUYUNGI ATETA NA WATENDAJI WAANDAMIZI COSTECH


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi ameitaka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuisaidia sekta binafsi kufanikisha matumizi ya teknolojia ya vifaa vya magari ya umeme ili kuhifadhi mazingira.

Dkt. Muyungi amesema hayo leo Jumatano (Januari 28, 2026) Jijini Dar es Salaam wakati wa kikao baina yake na Watendaji Waandamizi wa COSTECH waliofika ofisini kwake kuwasilisha andiko la kitaalamu la mwongozo wa kisera kuhusu uendelezaji wa teknolojia ya matumizi ya magari ya umeme.

Amesema matumizi ya teknolojia ya magari ya umeme imeshika kasi kwa sasa duniani na kuitaka COSTECH kuhakikisha inaandaa sera na miongozo mepesi kwa sekta binafsi ili iweze kushiriki kikamilifu katika mageuzi hayo.

Ukienda katika mataifa mengi ya Bara la Ulaya kwa sasa, yanatumia sana teknolojia hii na sekta binafsi ndiyo kinara, wakati umefika sasa kwa Tanzania kuhakikisha sekta binafsi inapewa msukumo na fursa ya uwekezaji katika miundombinu hii amesema Dkt. Muyungi.

Aidha amesema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kuweka mazingira wezeshi na kuhimiza Wizara za kisekta na Taasisi zinazohusika katika uendelezaji wa teknolojia hiyo zinaimarisha ushirikiano wa karibu na COSTECH.

Ameongeza kuwa uwepo wa matumizi ya teknolojia ya magari hayo yatarahisisha juhudi za uhifadhi na utunzaji wa mazingira kwa kuwa tayari Serikali imefanikisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya nishati ya umeme nchini.

Amesisitiza kuwa suala la matumizi ya teknolojia ya vifaa hivyo halina budi kwenda sambamba na kujenga uwezo kwa kuwapatia mafunzo wataalamu waliopo katika vyuo mbalimbali vya ufundi ikiwemo Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)
, Chuo cha Taifa cha Usafirshaji (NIT) na Taasisi ya Teknlojia Dar es Salaam (DIT).

Suala la Mafunzo na ujuzi ni muhimu, hivyo hatuna budi kuwawezesha na kupata maarifa ya kutosha yatakayosaidia katika usimamizi wa miundombinu ya teknolojia hizi amesema Dkt. Muyungi.

Amebainisha kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC) kitahakikisha kinashirikiana kwa karibu na COSTECH iili kuratibu vyema kuratibu matumizi ya teknolojia hizo ambayo ni kichocheo muhimu katika biashara ya kaboni.  

Kwa upande wake Meneja wa Ubunifu na Teknolojia- COSTECH, Dkt. Gerald Kafuku ameishukuru Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuendelea kutoa ushauri na maelekezo ya kitaalamu yaliyowekeza uandaaji wa andiko la mradi huo.

Dkt. Kafuku amesema taarifa ya andiko hilo limekusudia kuandaa mitaala ya kozi fupi na za muda mrefu zitakazotolewa katika vyuo vya ufundi ikiwemo VETA, NIT), DIT na Chuo cha Ufundi Arusha- ATC.

Aidha amesema COSTECH pia imepanga kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali wa kimataifa ikiwemo Serikali ya Norway hatua inayolenga kufanikisha upatikanaji wa mafunzo watakaosimamia miundombinu ya teknolojia hizo.

No comments:

Post a Comment