
Na Mwandishi Wetu,DAR
KATIBU MKUU wa Taifa wa Chama cha NLD Doyo Hassan Doyo January 6 mwaka huu 2026 ameongoza kikao cha Tathimini ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba mwaka 2025 cha Watendaji wa Makao Makuu na Afisi Kuu pamoja na Wagombea Wote.
Wagombea hao ni waliogombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo, ikiwa ni maandalizi ya vikao vya kikatiba vinavyotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Katika kikao hicho kimepitisha pia Taarifa ya maandalizi ya kugombea Ubunge Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma wakati tume itapotangaza rasmi kuanza mchakato wa kumpata mwakilishi wa Jimbo hilo .
Katibu Mkuu huyo aliwashukuru wananchi wote waliokiunga mkono chama chetu katika kampeni zake nchin kote wakati wa uchaguzi mkuu.
Hata hivyo alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wagombea wote waliogombea nafasi mbalimbali kote nchini nakuwataka wasife moyo na kujipanga kisawasawa katika chaguzi zijazo katika nchi yetu kwani hiyo ndyo njia pekee ya kuweza kushika Dola.

No comments:
Post a Comment