KASEKENYA AMPONGEZA MKANDARASI KWA KUKAMILISHA KAZI KWA WAKATI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, January 12, 2026

KASEKENYA AMPONGEZA MKANDARASI KWA KUKAMILISHA KAZI KWA WAKATI


Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amempongeza mkandarasi Rocktronic kwa kukamilisha ujenzi wa daraja la Minjingu katika mto Mulungu barabara ya Arusha- Babati kwa wakati na ubora.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara na madaraja mkoani Manyara Eng. Kasekenya amesema hatua ya kukamilisha miradi kwa wakati na ubora inaongeza imani ya Serikali kwa wakandarasi wa ndani na wasimamizi wa miradi wazalendo.

" Nia ya Serikali ni kuwawezesha wakandarasi na Wasimamizi wa ndani kujenga miradi mingi hivyo hatua ya kuikamilisha kwa wakati ni fursa ya kuaminika na kupewa miradi mingi zaidi", amesisitiza Eng. Kasekenya.

Amemtaka meneja wa Wakala wa Barabara TANROADS mkoa wa Manyara kuhakikisha daraja hilo linawekwa taa na kujengea kingo za daraja hilo ili zisiathiriwe na mafuriko kwa muda mrefu.

Kaimu meneja wa TANROADS mkoa wa Manyara Eng. Amon Mngulu amesema zaidi ya shilingi bilioni 6 zimetumika katika ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa mita 50 na hivyo kukamilika kwake kutaondoa mafuriko katika eneo hilo yaliokuwa yakikata barabara wakati wa mvua kubwa na kusababisha usumbufu kwa wananchi.

Naibu Waziri Kasekenya yuko katika ziara ya kukagua miundombinu ya barabara na madaraja katika mikoa ya Arusha na Manyara.




No comments:

Post a Comment