KIWANJA CHA NDEGE MSALATO KUKAMILIKA MWEZI MEI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, January 14, 2026

KIWANJA CHA NDEGE MSALATO KUKAMILIKA MWEZI MEI



Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amewataka wadau wote wanaosimamia ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Msalato kushirikiana ili ujenzi huo ukamilike ifikapo Mwezi Mei mwaka huu.


 Akizungumza jijini Dodoma, Januari 14, 2026 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi huo, Prof. Mbarawa amesema hatua ya ukamilishaji wa ujenzi (finishing), inahitaji umakini, kujali thamani ya fedha na ubora wa vifaa unaoendana na mahitaji.


 "Mameneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mamalaka ya Viwanja vya ndege (TAA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) pamoja na Zimamoto na Uhamimiaji shirikianeni kikamilifu ili vifaa na mifumo ya uendeshaji isomane na kurahisisha utendaji wa kazi kiwanjani hapo", amesisitiza Prof. Mbarawa.


 Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS mkoa wa Dodoma Eng. Zuhura Amani amesema wamejipanga kumsimamia kikamilifu mkandarasi anaejenga kiwanja hicho ili kikamilike kwa wakati.


 Nae, Mkurugenzi wa Kiwanja kiwanja hicho, Clemence Mbaruck amesema watahakikisha ujenzi unakamilika kwa viwango na tayari watumishi 170 tayari wameshahamishiwa Dodoma kwaajili ya kuanza kazi kwenye kiwanja hicho mara baada ya kufunguliwa rasmi.


 Zaidi ya shillingi bilioni 370 zinatumika kwaajili wa ujenzi huo na kukamilika kwake kutachochea ukuaji wa uchumi kwa wakazi wa Dodoma kwani kutaruhusu ndege aina mbalimbali za kitaifa na kimataifa kutua Kiwanjani hapo.









No comments:

Post a Comment