KUELEKEA KILELE CHA TUZO ZA SERENGETI WAZIRI MKUU NCHEMBA AFANYA ROYAL TOUR HIFADHI YA TAIFA ARUSHA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, January 31, 2026

KUELEKEA KILELE CHA TUZO ZA SERENGETI WAZIRI MKUU NCHEMBA AFANYA ROYAL TOUR HIFADHI YA TAIFA ARUSHA




Na Sixmund Begashe, Arusha


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba leo Januari 31, 2026 ametembelea Hifadhi ya Taifa Arusha ikiwa ni masaa machache kabla ya tukio kubwa la Serengeti Awards linalofanyika leo katika Hoteli ya Mt. Meru jijini Arusha.

Waziri Mkuu Nchemba ambaye anatarajiwa kuwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya Tuzo hizo, akiwa na mwenyeji wake ambaye ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) wametembelea pia eneo la maporomoko ya Maji Tululusia.

Ziara hiyo imehudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA. Amos Makalla, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi na watendaji walengine wa Wizara ya Maliasili na Utalii.




No comments:

Post a Comment