MHE. BALOZI OMAR AKAGUA JENGO JIPYA LA KISASA LA OFISI YA WIZARA YA FEDHA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, January 17, 2026

MHE. BALOZI OMAR AKAGUA JENGO JIPYA LA KISASA LA OFISI YA WIZARA YA FEDHA



Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (mwenye shati ya batiki), akisikiliza maelezo ya namna ya kutumia mifumo ya usalama na utambuzi iliyopo katika Jengo jipya la Wizara ya Fedha lililopo katika Mji wa Serikali-Mtumba, jijini Dodoma, kutoka kwa Afisa Tehama wa Wizara hiyo, Bw. Boniface Munishi (kulia), wakati alipotembelea Kukagua Jengo hilo la Ofisi la kisasa lenye ghorofa 9, akiambatana na Naibu Mawaziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) na Mhe. Laurent Luswetula (Mb) pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Fedha ikiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba.



Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) akiweka kadi katika mfumo wa usalama na utambuzi iliyopo katika Jengo Jipya la Wizara ya Fedha lililopo katika Mji wa Serikali-Mtumba, jijini Dodoma, ili kumruhusu kuingia, wakati alipotembelea na kukagua Jengo hilo jipya la Ofisi la Kisasa lenye ghorofa 9 kisasa, akiambatana na Naibu Mawaziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) na Mhe. Laurent Luswetula (Mb) pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Fedha ikiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba.



Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) akiongea jambo wakati akikagua eneo la Mgahawa katika Jengo Jipya la Kisasa la Ofisi za Wizara ya Fedha, lililopo katika Mji wa Serikali-Mtumba, jijini Dodoma, akiambatana na Naibu Mawaziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) na Mhe. Laurent Luswetula (Mb) pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Fedha ikiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba.



Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (mwenye shati ya njano), akisikiliza maelezo kuhusu eneo la lifti na matumizi yake kutoka kwa Msimamizi wa ujenzi wa Jengo la Wizara ya Fedha, Mhandisi. Japhet Mkwamira (kushoto), wakati akikagua Jengo jipya la kisasa la Ofisi za Wizara ya Fedha lililopo katika Mji wa Serikali-Mtumba, jijini Dodoma, akiambatana na Naibu Mawaziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (wa pili kushoto) na Mhe. Laurent Luswetula (Mb) (wa tatu kushoto). Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (watatu kulia) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (wa pili kulia).



Baadhi ya viongozi na watumishi wa Wizara ya Fedha, wakisiliza hotuba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (hayupo pichani), wakati akizungumza baada ya Kukagua Jengo jipya la kisasa la Wizara ya Fedha lililopo katika Mji wa Serikali-Mtumba, jijini Dodoma, akiambatana na Naibu Mawaziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) na Mhe. Laurent Luswetula (Mb) (hawapo pichani).



Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati), Naibu Mawaziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (wa tisa kushoto) na Mhe. Laurent Luswetula (Mb) (wa tisa kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa nane kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (wa nane kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa Wizara ya Fedha baada ya kukagua Jengo jipya la kisasa la Wizara ya Fedha lililopo katika Mji wa Serikali-Mtumba, jijini Dodoma.



Mwonekano wa Mandhari ya Jengo jipya la Kisasa la Wizara ya Fedha, lililopo katika Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma, ambalo Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amelitembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wake ambao umekamilika kwa asilimia 98, akiambatana na Naibu Mawaziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) na Mhe. Laurent Luswetula (Mb) pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Fedha ikiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)

No comments:

Post a Comment