ADEM na Mkoa wa Pwani Washirikiana Kuimarisha Uongozi na uwajibikaji wa Madiwani - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, January 17, 2026

ADEM na Mkoa wa Pwani Washirikiana Kuimarisha Uongozi na uwajibikaji wa Madiwani


Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mheshimiwa Petro Magoti akiwa kwenye picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dkt. Maulid J. Maulid, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe pamoja na Mwakilishi wa Madiwani wa Mkoa wa Pwani, mara baada ya kufunga mafunzo kwa Waheshimiwa Madiwani.

Mh. Magoti alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mheshimiwa Kunenge, katika hafla ya kufunga mafunzo hayo yaliyolenga kuwawezesha Madiwani kutambua na kutekeleza vyema majukumu yao ya uwakilishi wa wananchi katika kata zao. 

Mafunzo hayo yalihusisha Madiwani kutoka Halmashauri za Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Kisarawe.

No comments:

Post a Comment