
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa Fedha 2025/26 uliofanyika leo tarehe 21 Januari, 2026 katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akisisitiza jambo kwa Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa Fedha 2025/26 uliofanyika leo tarehe 21 Januari, 2026 katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi hiyo kwa mwaka wa Fedha 2025/26 uliofanyika leo tarehe 21 Januari, 2026 katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Mhe. Regina Qwaray alipokuwa akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa Fedha 2025/26 uliofanyika leo tarehe 21 Januari, 2026 katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.

Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa Fedha 2025/26 wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) wakati akifungua Baraza hilo leo tarehe 21 Januari, 2026 katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
Na Mary Mwakapenda-Dodoma
Tarehe 21.01.2026
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray amewataka Watumishi wa Umma kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi ikiwemo kutumia lugha nzuri na yenye staha ili kuimarisha amani na mshikamano.
Mhe. Qwaray ametoa maelekezo hayo wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa Fedha 2025/26 uliofanyika leo tarehe 21 Januari, 2026 katika Ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
Amesema, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wananchi ndio wenye Serikali, hivyo ni haki yao ya msingi kuhudumiwa kikamilifu.
“Kimsingi, huduma kwa wateja wetu ni lazima iwe bora inayokidhi matarajio yao na kwa wakati. Napenda kusisitiza suala la matumizi ya lugha nzuri na yenye staha kwa wateja na wananchi wote ili kujenga imani kubwa kwa Serikali yao na hivyo kuimarika kwa amani na umoja nchini,” amesisitiza Mhe. Qwaray.
Aidha, Mhe. Qwaray amewaelekeza watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI kuchambua kwa kina maeneo yaliyobainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala ya mwaka 2025 yanayohusu Ofisi hiyo ili kutekeleza ahadi zote zilizotolewa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wananchi kwa lengo la kuwaletea maendeleo na kukuza ustawi wao.
Amesema kazi inayofanywa na watumishi wa Ofisi hiyo ni nyeti kwani inagusa maisha ya kila siku ya Watanzania na ni kazi ambayo inahitaji watu waadilifu, wapenda haki na walio mfano mwema kwa jamii. Hivyo amewasisitiza kuzingatia misingi ya uzalendo, uadilifu, weledi, juhudi, maarifa na kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yenu.
Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imejielekeza katika kufuata Sheria na Misingi ya Utawala Bora ambapo inasisitiza juu ya haki na wajibu kwa kila Mtumishi wa Umma kwa Wananchi wote. “Ni imani yangu, Ofisi yetu itakuwa mstari wa mbele katika kutekeleza azma ya Serikali yetu kwa vitendo ili kupiga hatua kubwa ya maendeleo.” Ameongeza Mhe. Qwaray.
Wakati huo huo Mhe. Qwaray amewasisitiza Watumishi wa Umma kuendelea kutekeleza mifumo iliyojengwa na Serikali kwa lengo la kuboresha utendaji kazi katika Utumishi wa Umma.
Ameainisha baadhi ya mifumo hiyo ni pamoja na Mfumo wa Upimaji Utendaji kazi wa Watumishi wa Umma na Taasisi za Umma (e-Utendaji, Mfumo wa Tathmini wa Mahitaji ya Watumishi katika Utumishi wa Umma (HR Assessment) na Mifumo mingine.
Amesema mifumo hiyo mbali na kurahisisha utendaji kazi na kukuza uwajibikaji, inasaidia kwa kiwango kikubwa katika kuongeza ubora wa huduma kwa wananchi pamoja na kuongeza kasi ya utoaji wa huduma. “Hivyo, ni wazi kwamba ikitumika vizuri, tutaweza kwenda na kasi ambayo Mhe Rais wetu ametuelekeza.”Ameongeza Mhe. Qwaray.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, alimshukuru Naibu Waziri kwa kufungua Mkutano na kuahidi kusimamia kikamilifu utekelezaji wa malekezo aliyoyatoa kwa ustawi wa taifa.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kama ilivyo kwa Ofisi, Wizara na Taasisi nyingine za Umma, inawajibika kufanya Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi ambao pamoja na mambo mengine unatoa fursa kwa Wajumbe kujadili na kuidhinisha Mpango na Bajeti ya Ofisi kabla ya kuwasilishwa Bungeni pamoja na kujadili utekelezaji wa Bajeti baada ya kuidhinishwa na Bunge.
Baraza hilo la Wafanyakazi ni takwa muhimu la kisheria lililoelezwa katika Sheria ya Majadiliano ya Pamoja katika Utumishi wa Umma, Sura 105.

No comments:
Post a Comment