MTUMBA KUJENGWA VIWANJA VYA MTAANI VYA KUCHEZA USIKU-MAVUNDE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, January 24, 2026

MTUMBA KUJENGWA VIWANJA VYA MTAANI VYA KUCHEZA USIKU-MAVUNDE


Mbunge wa Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde ameeleza mpango wa ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya mpira wa kikapu na mpira wa miguu vya mtaani ambapo pia vitafungwa Taa ili kuruhusu michezo kufanyika muda wote.

Mavunde ameyasema hayo leo wakati akikabidhi vifaa vya Michezo kwa mitaa 104 iliyopo Jimbo la Mtumba kwa lengo la kuchochea michezo na kukuza vipaji Jimboni hapo.

“Tumepata wadau ambao tupo nao katika mazungumzo ya ujenzi wa viwanja vya michezo vya mtaani vya mpira wa kikapu na mpira wa miguu.

Viwanja hivi vitatumika mpaka majira ya usiku kwa kuwa vitakuwa na mfumo wa taa.

Ni mategemeo yangu kwamba uwepo wa viwanja na vifaa vya michezo vya kutosha vitasaidia kuchochea shughuli za michezo kwa vijana wa Mtumba”Alisema Mavunde

Wakati huo huo Mh. Mavunde amesema tayari ekari 12 za ardhi zimetengwa kata ya Chahwa kwa ajilo ya ujenzi wa kituo cha Michezo na kwasasa anaendelea kutafuta wadau ikiwemo TFF juu ya uendelezaji wa eneo hilo.

Sambamba na hilo Mh. Mavunde ametoa ahadi ya kuanzisha ligi ya kata kwa kata ili kuibua vipaji vya vijana wa mtumba.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Cde Charles Mamba amewataka viongozi wote kuhakikisha wanabuni na kuja na mkakati wa utekelezaji wa ahadi kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment