UMIKIDO WAFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI SANGU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, January 17, 2026

UMIKIDO WAFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI SANGU


Viongozi wa Umoja wa Wanahabari wa Vyombo vya Habari vya Mitandao ya Kijamii Mkoa wa Dodoma (UMIKIDO), wakiongozwa na Mwenyekiti wao Benny Majata,Januari 16, 2026 wamekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Mhe. Deus Sangu, katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, UMIKIDO imejitambulisha rasmi kwa Waziri Sangu tangu kuanzishwa kwake, sambamba na kueleza malengo ya kuunda umoja huo ikiwemo kuinua wanahabari wa mitandaoni, kuongeza ushirikiano na serikali pamoja na kutafuta nafasi za mafunzo na fursa za kiuchumi.

Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Afisa Uhusiano wa UMIKIDO, Daniel Mkate, na Mjumbe wa Umoja huo, Carlos Ngonya.

Akizungumza katika mazungumzo hayo, Waziri Sangu ameuhakikishia umoja huo kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kuwezesha vijana katika sekta mbalimbali, ikiwemo zile zinazogusa shughuli za habari na teknolojia.

Ameutaka UMIKIDO kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali na kusimamia nidhamu, weledi na ubunifu katika utendaji wao.

Aidha, Waziri Sangu ameahidi kushirikiana na umoja huo na kuushika mkono ili kuwawezesha vijana kuongeza kipato na kujijenga kiuchumi kupitia tasnia ya habari za mitandaoni.

#Sauti ya Mitandao, Mwelekeo wa Taifa


No comments:

Post a Comment