WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO SMZ AITEMBELEA BOT ZANZIBAR - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, January 17, 2026

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO SMZ AITEMBELEA BOT ZANZIBAR


Waziri wa fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Akil, amefanya ziara maalum katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Zanzibar kwa ajili ya kujadiliana masuala ya kimkakati yanayohusu usimamizi wa fedha na maendeleo ya uchumi wa Zanzibar.

Katika ziara hiyo, Dkt. Akil alisisitiza umuhimu wa kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidijiti katika ukusanyaji wa mapato ili kuhakikisha mapato hayo yanakusanywa kwa ufanisi na kwa usahihi.

Aliongeza kuwa matumizi ya teknolojia ya kidijiti yana mchango mkubwa katika kuimarisha uwazi, uwajibikaji na usimamizi bora wa fedha za umma.

Aidha, Waziri huyo alielekeza kuendelezwa kwa miradi ya maendeleo ya kimkakati kwa kuzingatia matumizi bora ya mapato ya ndani, akisisitiza kuwa mifumo ya kidijiti husaidia kupunguza utegemezi wa mikopo na kuimarisha maendeleo endelevu ya uchumi wa Zanzibar.

Dkt. Akil alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana kwa karibu na Benki Kuu ya Tanzania katika kuhakikisha uthabiti wa sekta ya fedha na kukuza uchumi jumuishi unaowanufaisha wananchi.

Ziara hiyo iliyofanyika tarehe 14 January 2026 ni ya kwanza kwa Waziri huyo tangu kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo.



No comments:

Post a Comment