
Na Witness Masalu WMJJWM-Dodoma
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ametoa rai kwa watumishi wa Wizara hiyo kuwekeza mioyo, nguvu na akili zao katika kuwatumikia wananchi kwa haki na weledi ili kupata matokeo yenye tija .
Dkt Gwajima ameyasema hayo katika kikao cha mwanzo wa mwaka baina yake na Watumishi wa Wizara hiyo tarehe 16 Januari 2026 katika Ofisi za Wizara ziliziopo Mji wa Serikali-Mtumba Mkoani Dodoma.
Dkt Gwajima amewapongeza watumishi hao kwa kazi nzuri waliyoifanya mwaka 2025 na kuwasisitiza kuongeza kasi na ukaribu wa kuwahudumia wananchi kwani dhana za kufanyia kazi wanazo tayari.
“Tunaanza mwaka huu tukiwa na dhana ya kufanyia kazi wa Wizara hii kama ilivyochapishwa kwenye gazeti la Serikali na natumaini watumishi wote wataweza kuelewa dhana hiyo lakini vile vile tunatakiwa kutembea na dira ya Maendeleo ya 2025-2050 ili kuhakikisha maono ya Mhe Rais Samia kwa nchi yetu yanatekelezwa kikamilifu”amesema Dkt. Gwajima.
Aidha Dkt. Gwajima amewasihi watumishi hao kuweka pembeni changamoto zao na kufanya kazi kwa umoja pamoja na kusimamia Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM 2025-2030) katika utekelezaji wa majukumu yao na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amewasisitiza watumishi hao kuishi kwa upendo baina yao wenyewe lakini pia kuwahudumia wananchi kwa upendo wa dhati.
“Upendo wa dhati unahitajika ili kupunguza ugumu wa kulichukulia jukumu la kuwahudumia wananchi kama ni zito hivyo uzalendo wa dhati unahitajika kwa ajili ya maslahi ya jamii na taifa letu kwa ujumla". amesema Mhe. MaryPrisca.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amesema vikao hivyo baina ya viongozi na watumishi vina tija na umuhimu katika utumishi wa umma na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri.







No comments:
Post a Comment