PROF. SHEMDOE KUZIFANYIA KAZI CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHARA SOKO LA MABIBO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, March 5, 2026

PROF. SHEMDOE KUZIFANYIA KAZI CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHARA SOKO LA MABIBO.



Na OWM-TAMISEMI, Dar es Salaam


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI, Mhe .Prof. Riziki Shemdoe amekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Mabibo kwa lengo la kutatua mgogoro uliopo katika soko hilo.

Akizungumza na Wafanyabiashara hao mapema leo Machi 04, 2026 katika ofisi ndogo za OWM-TAMISEMI Magogoni Jijini Dar es Slaam, Prof. Shemdoe amesema yuko tayari kutatua changamoto za wafanyabiashara walizoziwasilisha kwake ambazo ni pamoja na kurejeshwa katika soko hilo baada ya kuzuiliwa na uongozi wa soko, kurudishiwa vizimba vya biashara na ombi la kutaka usimamizi wa soko hilo kujeshwa kwa wafanyabiashara wa Mabibo.

Prof. Shemdoe ameahidi kushughulikia maombi ya wafanyabiashara hao ndani ya wiki mbili na kuwaahidi kukutana tena baada ya kupata ufumbuzi wa suala hilo.

Aidha, Prof. Shemdoe ameteua kamati Maalum ya kushughulikia suala hilo chini ya uenyekiti wa Naibu Katibu Mkuu anayeshugulikia Miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila.

Hatua ya Prof. Shemdoe inafuatia maelekezo aliyoyatoa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba baada ya wafanyabiashara hao kuwasilisha changamoto hizo kwake.





No comments:

Post a Comment