TEHAMA YARAHISISHA USAJILI NA UHAMISHO WA WANAFUNZI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, March 5, 2026

TEHAMA YARAHISISHA USAJILI NA UHAMISHO WA WANAFUNZI


Mfumo wa Kidigitali wa usajili wa wanafunzi wa shule za msingi (PReM) na usajili wa watahiniwa wa sekondari (PReMS) umetajwa kuwa mbinu sahihi ya kurahisisha utendaji wa baraza ikiwemo kurahisisha usajili, uhamisho wa wanafunzi na upangaji mipango ya maendeleo ya Elimu.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, wakati wa ziara yake katika ofisi za Baraza la Mitihani la Taifa NECTA Machi 4, 2026.

Amesema kuwa Baraza hilo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1973, limekuwa mhimili wa ubora wa elimu na kusimamia mitihani kwa haki na weledi na sasa TEHAMA imekujabkuleta mapinduzi katika utendaji na huduma.

Amesema maendeleo ya teknolojia yamesaidia kupunguza gharama za uchapaji wa vyeti ndani ya nchi na kuongeza usalama wa nyaraka, pamoja na uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma zaidi ya 682,000 ulioimarisha uadilifu wa taaluma. 

Akizungumzia maandalizi ya Mkutano wa Mabaraza ya Mitihani ya Afrika (AEAA) utakaofanyika Arusha Agosti 2026 wenye kaulimbiu isemayo “Rethinking Educational Assessment in the Age of Artificial Intelligence,”amesema ni fursa muhimu kwa Tanzania kuonesha ubora wake katika upimaji barani Afrika lakini pia ni fursa ya kubadilishana uzoefu kuhusu tathmini za wanafunzi na matumizi ya Teknolojia ikiwemo akili Unde katika eneo hilo.

Pia Mhe. Wanu amesema Serikali itaendelea kugharamia ujenzi wa kituo cha umahiri na utafiti kinachojengwa Mikocheni, jijini Dar es Salaam ambacho uwekezaji wake ni Sh. bilioni 8.9 pamoja na upanuzi wa kiwanda cha uchapaji kwa ajili ya kuimarisha kazo ya utahini na upimaji. 


Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Mohamed, amesema Baraza limeendelea kusimamia mitihani kwa wakati kwa kuzingatia kalenda iliyoidhinishwa, huku likijiandaa kuwapokea zaidi ya watahiniwa milioni 6.6 ifikapo mwaka 2027.

No comments:

Post a Comment