WAUMINI WA KANISA KATOLIKI ZAIDI YA 100 WAWASILISHA MALALAMIKO UBALOZI WA VATICAN - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, January 5, 2026

WAUMINI WA KANISA KATOLIKI ZAIDI YA 100 WAWASILISHA MALALAMIKO UBALOZI WA VATICAN



Zaidi ya waumini 100 wa Kanisa Katoliki leo wamewasilisha barua rasmi ya malalamiko katika Ubalozi wa Vatican nchini Tanzania, wakilalamikia uongozi wa Askofu Mkuu Protase Kardinali Ruwa’ichi na Padri Charles Kitima.

Barua hiyo imewasilishwa kwa kufuata taratibu za kidiplomasia, ikibeba madai yanayohusisha ukiukwaji wa maadili ya uongozi wa Kanisa, matumizi mabaya ya mamlaka ya kiroho pamoja na kauli zinazodaiwa kuwavunjia heshima baadhi ya waumini.

Hatua hiyo inakuja wakati ambapo kumekuwepo na mvutano ndani ya Kanisa Katoliki, baada ya waumini kadhaa kujitokeza hadharani kupinga misimamo ya baadhi ya viongozi wa kanisa hilo.

Waumini hao wanadai viongozi hao kujikita zaidi katika masuala ya kisiasa, badala ya kuzingatia na kusimamia maadili ya Kanisa kwa mujibu wa mafundisho ya vitabu vitakatifu.

Hadi sasa, uongozi wa Kanisa Katoliki haujatoa tamko rasmi kujibu madai hayo.




No comments:

Post a Comment