Na: Dickson Bisare -Okuly Blog -Arusha
Ajali ya barabarani imehusisha basi la abiria na gari aina ya Hiace katika eneo la kwa Idd, wilayani Arumeru mkoani Arusha, tukio lililotokea leo na kuzua taharuki miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa za awali zilizopatikana, ajali hiyo imehusisha vyombo hivyo viwili kugongana katika mazingira ambayo chanzo chake bado hakijathibitishwa rasmi.Hadi sasa, mamlaka husika zinaendelea kukusanya taarifa ili kubaini kilichosababisha ajali hiyo.
Mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wamesema walishuhudia taharuki mara baada ya magari hayo kugongana,huku juhudi za awali za uokoaji zikifanyika kwa kushirikiana na wasamaria wema kabla ya vyombo vya usalama kufika eneo la tukio.
Idadi ya majeruhi au madhara yaliyotokana na ajali hiyo bado haijatolewa rasmi na mamlaka za usalama barabarani.Taarifa zaidi zinatarajiwa kutolewa mara baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.
Eneo la Idd ni miongoni mwa maeneo yenye shughuli nyingi za usafiri,hali inayoongeza umuhimu wa tahadhari kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara.
Okuly Blog tunaendelea kufuatilia kwa karibu tukio hili ili kuwapatia taarifa sahihi na za kina kuhusu chanzo cha ajali pamoja na hali ya wahusika.
Endeleeni kufuatilia ukurasa wetu wa Instagram na mitandao yetu mingine ya kijamii kupitia Okuly Blog kwa taarifa zaidi zitakazokuwa zinatolewa kadri tunavyozipata kutoka kwa mamlaka husika.


No comments:
Post a Comment