Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 23, 2026 amezindua Shule ya Sekondari Sinya iliyopo katika Kata ya Sinya, Kijiji cha Leremeta, Wilaya ya Longido mkoani Arusha.
Ujenzi wa shule hiyo umegharimu shilingi bilioni 1.2 kutoka Serikali Kuu, SEQUIP, TASAF na Mapato ya Ndani ya Halmashauri, pamoja na mchango wa wananchi wa shilingi milioni 34.
Shule hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza upatikanaji wa elimu ya sekondari, kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule zilizopo na kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa jamii ya Sinya na maeneo jirani.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Dkt. Mwigulu amewataka wanafunzi katika shule hiyo wasome kwa bidii ili waweze kunufaika na fursa za elimu ambazo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameziweka kwa watoto wa kitanzania ikiwemo proramu ya ufadhili wa masomo ya ‘Samia Scholarship’.









No comments:
Post a Comment