BALOZI OMAR: BARAZA LA MASOKO YA MITAJI LITOE ELIMU YA MAJUKUMU YAKE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, February 20, 2026

BALOZI OMAR: BARAZA LA MASOKO YA MITAJI LITOE ELIMU YA MAJUKUMU YAKE

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiagana na Mwenyekiti wa Baraza la Masoko ya Mitaji Mhe. Jaji Dkt. Ntemi Kilekamajenga, baada ya kumalizika kwa kikao kati yao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akieleza umuhimu wa Baraza la Masoko ya Mitaji katika kutatua changamoto za Masoko wakati wa kikao kati yake na Mwenyekiti wa Baraza la Masoko ya Mitaji Mhe. Jaji Dkt. Ntemi Kilekamajenga, kilichofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akisikiliza maelezo ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, wakati wa kikao na Uongozi wa Baraza la Masoko ya Mitaji kilichofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Masoko ya Mitaji Mhe. Jaji Dkt. Ntemi Kilekamajenga, akizungumza kuhusu lengo la kuanzishwa kwa Baraza hilo wakati wa kikao na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (hayupo pichani) kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha Bi. Dionisia Mjema, akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (hayupo pichani) na Uongozi wa Baraza la Masoko ya Mitaji Mhe. Jaji Dkt. Ntemi Kilekamajenga kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Natu El-Maamry Mwamba.


(Picha na Kitengo cha Mawasilino Serikalini Wizara ya Fedha Dar es Salaam)


Na. Josephine Majura na Peter Haule, WF, Dar es Salaam



Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameitaka Mamlaka hiyo kutoa elimu kuhusu Baraza hilo ili wadau wengi waweze kulitumia kutatua changamoto zao.

Mhe. Balozi Omar, ametoa maelekezo hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Baraza la Masoko ya Mitaji ukiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. Jaji Dkt. Ntemi Kilekamajenga, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.

Aidha, alieleza dhamira ya Serikali ya kuendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji ili kuvutia mitaji na kukuza maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Masoko ya Mitaji, Mhe. Dkt. Ntemi Kilekamajenga, amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa Baraza hilo ni kuwa na jukwaa maalumu kwa ajili ya usikilizwaji wa migogoro inayohusu Masoko ya Mitaji.

Alisema kuwa Baraza hilo lina Mamlaka pia ya kusikiliza migogoro inayotoka kwenye Soko la bidhaa yakiwemo masuala ya stakabadhi gharani.

Kikao hicho kimehudhuliwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Msajili wa Baraza la Masoko ya Mitaji, Dkt. Martin Kolikoli na Kaimu Kamishna Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha Bi. Dionisia Mjema.

No comments:

Post a Comment