BARABARA YA MOMBO-LUSHOTO KM 32 KUPANULIWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, February 18, 2026

BARABARA YA MOMBO-LUSHOTO KM 32 KUPANULIWA



Serikali imekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya upanuzi wa barabara ya Mombo- Lushoto km 32.

Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amesema hayo katika ziara ya Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba inayoendelea wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Amesema hatua hiyo ni muendelezo wa mikakati ya Serikali kuchochea biashara ya utalii,
kilimo cha chai, mboga,matunda na mbao wilayani Lushoto.

"Mhe, Waziri Mkuu Wizara ya ujenzi kupitia Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), tumejipanga pia kuijenga kwa lami barabara ya Soni-Bumbuli-Dindira-Old Korogwe km 74 ili kuziunganisha Wilaya za Lushoto na Korogwe kwa barabara ya lami inayopita milimani katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya biashara", amesema Eng. Kasekenya.

Amesema awamu ya kwanza itahusisha eneo la Soni-Bumbuli km 22 upande wa Lushoto na eneo la Kwameta- Kwashemshi Km 9.3 upande wa Korogwe.

Waziri Mkuu Dkt. Amehitimisha ziara yake ya siku tano mkoani Tanga kwa kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya za Handeni, Kilindi, Pangani,Muheza, Mkinga, Tanga, Korogwe na Lushoto akisisitiza wananchi kutunza na kuilinda miundombinu ili iwanufaishe kiuchumi na kijamii.




No comments:

Post a Comment