
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema haikubaliki kwa watendaji wa Serikali kupokea fedha za utekelezaji wa miradi kisha kushindwa kuzitumia kwa wakati, hali inayosababisha wananchi kukosa huduma na maendeleo yaliyokusudiwa.
Dkt. Mwigulu ametoa kauli hiyo leo Februari 18, 2026, alipokuwa akizungumza na wananchi wa Ndungu, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, ambapo ameanza ziara ya kikazi mkoani humo.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akifanya juhudi kubwa kutafuta fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo, hivyo ni wajibu wa watendaji kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa uadilifu na kwa wakati ili wananchi wanufaike.
Aidha, Waziri Mkuu amemtaka Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Reuben Kwagilwa, kufanya ufuatiliaji wa kina kubaini iwapo kuna baadhi ya watendaji wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wanaotumia makampuni yao binafsi kutekeleza miradi na kushindwa kusimamia ipasavyo utekelezaji wake.
Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu amesema Rais Samia ameelekeza kuwa kila kwenye eneo halali la Mtanzania lisichukukiwe bure kwa kuwa huo ndio urithi wake.
Waziri Mkuu pia amekagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Ndungu–Mkomazi yenye urefu wa kilomita 36 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mradi unaolenga kuboresha miundombinu ya usafirishaji na kuchochea shughuli za kiuchumi katika ukanda huo.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ameziagiza Serikali katika vijiji kuhakikisha wanazingatia matumizi bora ya ardhi. “Kila mmoja aheshimu matumizi bora ya ardhi, na wote wanaofanya kiburi tutashughulika nao maana wanatupeleka katika kuondoa upendo miongoni mwetu”





No comments:
Post a Comment