Na; Dickson Bisare Okuly Blog -Dar Es Salaam
Msajili wa vyama vya michezo taifa (bmt), wakili Abel M. Ngilangwa, amethibitisha kuwa marekebisho ya katiba ya Simba Sports Club yamekamilika rasmi baada ya kufanyiwa uchambuzi na tathmini kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza mbele ya Wanahabari jijini dar es salaam, msajili huyo alisema hatua zote za kisheria zimezingatiwa katika mchakato wa kupitia na kuboresha katiba hiyo ili kuhakikisha inakidhi matakwa ya kisheria na kanuni za usajili wa vyama vya michezo nchini.
Ngilangwa alieleza kuwa marekebisho hayo yamefanyika kufuatia tamko la waziri wa habari,utamaduni, sanaa na michezo, Mhe. Paul Christian Makonda,aliyesisitiza umuhimu wa simba Sc kuwa na katiba inayoendana na sheria na miongozo ya sasa ya uendeshaji wa klabu za michezo.
Kwa mujibu wa msajili, uchambuzi,uthathimini na uhakiki wa vipengele vyote vya katiba hiyo umekamilika,na kilichobaki ni kuikabidhi rasmi kwa uongozi wa Simba Sc baada ya kuhakikisha kuwa marekebisho yote yaliyokubaliwa yameingizwa katika fomu maalum ya mwisho.
Alifafanua kuwa kabla ya kukabidhiwa kwa hati hiyo, uongozi wa Simba Sc unatakiwa kuhakiki kwa mara ya mwisho ili kuthibitisha kuwa maudhui yaliyomo ndiyo marekebisho halali yaliyokubaliwa kati ya pande husika wakati wa mchakato huo.
Hatua hiyo inalenga kuimarisha uwajibikaji,uwazi na uendeshaji bora wa klabu hiyo kongwe nchini, sambamba na kulinda maslahi ya wanachama na wadau wake.
Marekebisho hayo yanatarajiwa kuipa simba Sc mwelekeo mpya wa kiuongozi na kisheria,huku yakizingatia matakwa ya mamlaka za usajili wa vyama vya michezo nchini.





No comments:
Post a Comment