INSP NDUNGURU AKEMEA UTORO KWA WANAFUNZI WA NGHONG'ONGNHA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, February 12, 2026

INSP NDUNGURU AKEMEA UTORO KWA WANAFUNZI WA NGHONG'ONGNHA.


Wanafunzi wa shule ya sekondari Nghong'ongnha Jijini Dodoma wametakiwa kuzingatia masomo wanayofundishwa na walimu na kuepuka tabia ya utoro shuleni inayo sababisha wanafunzi kujiunga na makundi rika ya uhalifu pamoja na matumizi ya dawa za kulevya.

Kauli hiyo imetolewa februari 11, 2026 na Polisi kata wa kata hiyo Mkaguzi wa Polisi Yohanes Nduguru wakati akitoa elimu kwa wanafunzi ambapo amesisitiza suala la nidhamu uadilifu pamoja na uzalendo.

Aidha, Ndunguru ameeleza madhara yatokanayo matumizi ya dawa za kulevywa kwa wanafunzi ikiwemo kukatisha ndoto walizo nazo ambazo husababishwa na kujiunga makundi ya uhalifu ikiwemo wizi na uporaji

Kwa upande wao wanafunzi wameahidi kutoa taarifa kwa uongozi wa shule na kwa Jeshi la Polisi dhidi ya wanafunzi ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo matumizi ya dawa za kulvya (bangi) wauzaji dawa hizo majumbani na shuleni ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Vilevile uongozi wa shule umepongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kuendelea kutoa elimu kwa wanafunzi hao ambayo imekuwa ikileta tija kwa wanafunzi ikiwemo kubadilika kifikra na kitaaluma jambo linalo pelekea kuongezeka kwa ufaulu shuleni hapo.

No comments:

Post a Comment