MAVUNDE AZINDUA KISIMA CHA MAJI MSALATO, AWAHIMIZA WANANCHI KUKILINDA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, February 16, 2026

MAVUNDE AZINDUA KISIMA CHA MAJI MSALATO, AWAHIMIZA WANANCHI KUKILINDA



Na Mwandishi Wetu - Dodoma


Mbunge wa Jimbo la Mtumba, Anthony Mavunde, amezindua kisima cha maji katika Mtaa wa Msalato (Ubalozi wa Catherine Mwajoka) kwa ajili ya matumizi ya wananchi, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ahadi aliyoitoa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kuhusu kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mheshimiwa Mavunde amesema utekelezaji wa mradi huo ni matokeo ya dhamira ya kuondoa changamoto ya maji iliyokuwa ikiikabili jamii ya eneo hilo kwa muda mrefu.

Amewataka wananchi wa Msalato kulinda na kuitunza miundombinu ya kisima hicho ili kiweze kudumu na kuwanufaisha kizazi cha sasa na kijacho.

Aidha, ameahidi kuendelea kushirikiana na wananchi katika kutatua changamoto nyingine za maendeleo katika jimbo hilo.

Katika hafla hiyo, Mheshimiwa Mavunde pia aliwashukuru wananchi wa Msalato kwa imani kubwa waliyoionesha kwa kumpigia kura Samia Suluhu Hassan, yeye kama Mbunge pamoja na Diwani wao wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Amesema ushirikiano na mshikamano wa wananchi ni msingi muhimu wa kuharakisha maendeleo na utekelezaji wa miradi ya kijamii katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Mtumba.



No comments:

Post a Comment