
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Shirika la ASK-International imehitimisha mafunzo maalum ya ubebaji bora wa wagonjwa wasioweza kujimudu wenyewe, wakiwemo wagonjwa waliopooza, wazee wanaohitaji msaada wa kubebwa, pamoja na waliopata ajali au kuumia vibaya ili kuwaepusha na athari nyingine za kiafya wakati wa matibabu.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Ukunga na Uuguzi Hospitalini hapo, Bi. Redemptha Matindi, amesema hospitali ilibaini kuwepo kwa pengo kubwa katika eneo la ubebaji na uhamishaji wa wagonjwa ambapo meeleza kuwa hatua hiyo italeta nafuu si kwa wagonjwa pekee bali pia kwa wauguzi, kwa kuwa watatumia mbinu za kisasa na salama zaidi bila kujiweka katika hatari ya kupata maumivu au majeraha kazini.
Ameongeza kuwa lengo kuu ni kupunguza matatizo yanayoweza kujitokeza wakati wa mgonjwa akihudumiwa, ikiwemo maumivu makali, vidonda vinavyotokana na kulala muda mrefu, hivyo wakufunzi walijikita katika kutoa mbinu bora za kumhamisha mgonjwa kutoka kitanda kimoja kwenda kingine, kutoka kwenye kiti mwendo kwenda kitandani au kinyume chake, bila kumletea madhara mgonjwa wala mhudumu wa afya.
Aidha wauguzi kutoka wodi mbalimbali Muhimbili, ndugu wa wagonjwa wanaohitaji msaada wakiwa nyumbani.








No comments:
Post a Comment