Naibu Katibu Mkuu Maji awataka Wajumbe Bodi za Mamlaka za Maji kuwa chachu ya mabadiliko - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, February 23, 2026

Naibu Katibu Mkuu Maji awataka Wajumbe Bodi za Mamlaka za Maji kuwa chachu ya mabadiliko


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Bi. Rose Zacharia amewataka wajumbe wa Bodi za Wakurugenzi wa Mamlaka za Majsafi na Usafi wa Mazingira nchini kuwa chachu ya mabadiliko chanya katika utoaji huduma kwa wananchi.

Ametoa wito huo akiwasilisha Salam za Wizara ya Maji katika Mkutano wa Wajumbe wa Bodi hizo jijini Arusha.

Amesema jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha huduma ya majisafi na salama inawafikia Watanzania wote zinaonekana wazi hivyo wajumbe wanapaswa kumuunga mkono kwa kufanya kazi kwa kujituma zaidi.

Amesema Wizara ya Maji inayo imani kubwa na wajumbe hao hivyo majadiliano ndani ya kikao kazi hicho yalenge kupiga hatua mbele katika kuyafikia malengo.

Kikao cha Wajumbe wa Bodi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini kinatarajiwa kufunguliwa Februari 24, 2026.

Mgeni Rasmi atakayefungua ni Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb)


No comments:

Post a Comment