
Baada ya Ofisi ya Makamu wa Rais kutoa waraka wa katazo kwenye taasisi zote zinazolisha watu zaidi ya mia moja nchini kuachana na matumizi ya Nishati isiyo safi na kuhamia kwenye nishati safi ya kupikia, Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Sakura yaingia kwenye Orodha ya Taasisi zinazotumia Nishati Safi ya Kupikia.
Hayo yametabanaishwa Februari 05, 2026 wakati timu ya wataalam kutoka Wizara ya Nishati ilipotembelea shuleni hapo kukagua mradi wa LPG na GAS Vaporizer unaofadhiliwa na Shirika la KAGLA Eco Friendly wakishirikia na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan, JICA.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Shule hiyo Bw. Thomas Rubeni amesema Shule ipo milimani na eneo hili kuna baridi kali wakati wa asubuhi, jioni na msimu wa Masika ambapo hali ya hewa hiyo huathiri afya za wanafunzi hivyo uwepo wa mfumo wa gesi utasaidia wanafunzi kupata maji moto na kupunguza hewa ukaa kwani matumizi ya kuni yanachangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa hewa ya ukaa kwenye mazingira.
Aliongeza kuwa uwepo wa nishati safi ya kupikia utawasaidia wapishi kupika kwa urahisi na kwa wakati"
Kwa upande wake Mpishi wa shule hiyo Rahel Elisante ameeleza kuwa toka wameanza kutumia ya gesi wameepukana na adha mbalimbali za kimazingira na kiafya.
“ Tunafurahi na tunashukuru kwa kupata gesi kwani mwanzo tulikuwa tunapata shida mfano wakati wa baridi na mvua kuni zinakua mbichi na kutoa moshi na kuchelewesha kuiva chakula kwa wakati ila sasa hivi tunatumia gesi ambayo inarahisisha kazi yetu ya kila siku’ Bi. Elisante.
Naye mwakilishi wa wanafunzi Lidya Lebayo wa Sakura amesema upatikanaji wa gesi utawasidiia kupata maji moto ya uhakika katika vipindi vyote wawapo shule na pia kupata chakula kitamu kisicho na harufu ya moshi.







No comments:
Post a Comment